SEHEMU YA PILI YA TAMTHILIA YA "HUBA" KURUKA MWANZONI MWA MWAKA 2017

MSANII Irene Paul ambaye sasa amejikita kwenye tamthilia ameeleza furaha yake kwa tamthilia anayoshiriki ya “Huba” ambayo sehemu ya pili itaanza kurushwa hewani mwanzoni mwa mwaka ujao.

“Wanaofuatilia tamthilia watakuwa wameshaanza kuishuhudia sehemu ya kwanza ya “Huba” huku mimi na wasanii wenzangu tukiendelea kurekodi sehemu ya pili ambayo itaanza kuruka hewani mwanzoni mwa mwaka ujao,” alisema.

Alisema kuwa ameamua kujikita kwenye tamthilia baada ya kuombwa kufanya hivyo na watu wake wa karibu na anaamini kwamba tamthilia zina nafasi kubwa kwenye vituo vya televisheni.


Tamthilia hiyo inashirikisha wasanii nyota kama Muhogo Mchungu, Riyama Ally, Rammy Galis, Mutrah, Kidoa Salum Getrude Mwita na wengine kadhaa ambao wamekuwa wakishiriki katika filamu mbalimbali.

No comments