SERGIO AGUERO KILOMITA ELFU NANE NYUMA YA DIEGO COSTA

UPO uwezekano kuwa takwimu zina nafasi kubwa ya kutoa majibu ya ukweli kuliko kinyume chake.

Kama unabisha sikiliza takwimu za mastaa wawili wa (Chelsea) Diego Costa na (Manchester City) Sergio Aguero.

Wataalam hawa wa kutikisa nyavu za lango Ligi Kuu England walikuwa na mabao 20 kwa jumla yao, huku kila mmoja akigusa nyavu mara 10.

Lakini kabla ya mechi ya jana baina ya timu hizo, Costa alikuwa na mchango mkubwa wa mafanikio kwa timu yake kuliko Aguero wa Manchester City.

Costa alikuwa ametoa pasi nne za mabao na kutengeneza nafasi 22 za kufunga, wakati Aguero hajatoa pasi yoyote ya bao kwa wenzake.


Pia Costa alikuwa amewania mipira mingi ya kichwa kuliko Aguero.

No comments