SHAMSA FORD ASEMA HATAUSAHAU MWAKA 2016

WAKATI mwaka 2016 unamalizika muda si mrefu, mwigizaji Shamsa Ford amesema kuwa ana jambo kubwa ambalo ataendelea kulikumbuka katika maisha yake, lililomtokea katika mwaka huu.

“Uhumba wetu ulikumbana na changamoto nyingi ikiwemo watu kunikatisha tamaa kwa kuniambia kuwa siwezi kuolewa na pia mchmba wangu kuambiwa kuwa wasanii hawafai kuolewa lakini bahati nzuri tumefunga ndoa, tukio hili sitalisahau,” alisema.

Alisema kuwa yeye na Chidi, Mapenzi ambaye sasa ni mume wake, wasingekuwa na msimamo wasingefikia hatua ya kufunga ndoa kwa madai kwamba uchumba wao ulizunguukwa na mambo ya kukatisha tamaa.


“Njama zote za kutaka kutuvurugia zilikwama na sasa tuko pamoja tunakula maisha na ninatamani Mungu akinijalia nizae hata watoto kumi kwa sababu ninapenda sana watoto,” alisema Shamsa.

No comments