SHILOLE AAPA KUIHESHIMU BONGOMUVI MILELE

STAA wa kike wa muziki wa Kizazi Kipya, Zuwena Mohammed “Shilole” amesema ataendelea kuuithamini Bongomuvi kwakuwa ndio mizizi yake katika sanaa na ndio iliyomfanya ajulikane kiasi kwamba alipoamua kugeukia muziki ikawa rahisi kwake kufanikiwa.

“Nilianza kujulikana ndani ya Bongomuvi kisha nikageukia muziki wa Kizazi Kipya na ilikuwa ni rahisi kwangu kupata umaarufu ambao umenifanya niwe na mafanikio makubwa,” alisema Shishi.

Alisema, kujenga nyumba na kuishi maisha mazuri ni hatua kubwa sana kwake na anaamini Bongomuvi imechangia kwa kufanya watu wamfahamu na hata alipoamua kugeukia upande wa pili ilikuwa ni mteremko kupata mafanikio.


“Wakati ninatoka Bongomuvi kuingia katika muziki wa kizazi kipya, sikuwa na mafanikio kama niliyonayo sasa lakini siwezi kudharau fani hiyo kwasababu ndio iliyonifungulia njia,” alisema.

No comments