Habari

SIKINDE WAIPASUA KISUMA MWEMBEYANGA WAKIWA NA “BITCHUKA WAO”

on

ZILE tetesi za kwamba huenda
mkongwe Hassan Bitchuka akaondoka Mlimani Park Sikinde na kutua Msondo Ngoma,
jana Jumamosi zilidhihirika ni uzishi usio na maana pale nguli huyo alipoendelea
kushiriki kikamilifu na wanamuziki wenzie jukwani.
Kwa kuwa tetesi hizo
zilishasambaa na kuanza kuonekana kama ni ukweli uliojificha, Saluti5 iliamua
kutinga ukumbi wa Kisuma Mwembeyanga ili kujionea “live” hali halisi, ambako
kinyume na matarajio ya wengi, Bitchuka alipanda jukwaa la Sikinde na kututumbuiza
mwanzo mwisho.
Tofauti na kawaida yake, jana
Bitchuka alipopanda jukwaani alimpumzisha mwimbaji wao kiraka Abdallah Hemba
kwa muda mrefu na kuamua kusimama mwenyewe kwa kuimba kwa zaidi ya robo tatu ya
muda wa shoo hiyo iliyohudhuriwa na mashabiki wengi zaidi.

Vibao kama vile “Kelele za Paka”,
“Mfaume Waniliza”, “Supu Umeitia Nazi”, “Ni Nani”, “Bubu Ataka Kusema” na “Wali
Nazi”, vilionekana kuwasisimua mno mashabiki wengi, hasa kutokana na namna mwimbaji
huyo alikuwa akiviimba kwa hisia kali.
PATA PICHA 10 ZA NAMNA MAMBO YALIVYOKUWA:
Mkongwe Musemba wa Minyugu (kushoto), akiimba kwa hisia sambamba na chipukizi Said Msakara
Mwimbaji kiraka Abdallah Hemba akilalamika kwa sauti yake nzito mbele ya mashabiki wao
Nguli wa kupuliza Saxaphone, Shaaban Lendi akiongeza ladha kikamilifu na kuufanya muziki uzidi kunoga
Hapa mwimbaji Hassan Kunyata akiimba huku akinengua kwa madaha 
Karama Reggesu (kushoto), akiimba pamoja na mkali mwenzake, Hemba
Mcharazaji mahiri wa gitaa zito la Bass, Tony Karama akisisimua mashabiki kwa midundo ya nguvu
Hasan Bitchuka akiwajibika jukwaani
Said Msakara nae akionyesha uhodari wake wa sauti
Karama Reggesu akiwamaliza mashabiki kwa kitu “Wali Nazi”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *