SOKA HALINA ADABU …LIVERPOOL YAKALISHWA 4-3 NA AFC BOURNEMOUTH


LICHA ya kuongoza 2-0 hadi mapumziko, Liverpool ikajikuta inakubali kichapo cha 4-3 kutoka kwa Bournemouth.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya England Sadio Mane aliifungia Liverpool bao la kuongoza dakika ya 20 kabla ya Divock Origi hajatupia la pili dakika mbili baadae.

Callum Wilson akapunguza kwa kuifungia Bournemouth bao la kwanza dakika ya 56 lakini dakika nane baadae Liverpool wakatanua wigo kwa kupachika goli tatu mfungaji akiwa Emre Can.


Kibao kikageuka dakika ya 76, 79 na 90 kwa Bournemouth kufunga mfululizo kupitia kwa Ryan Fraser, Steve Cook na Nathan Ake.

No comments