TAARIFA ZA “KUMCHAFUA” ZAMKERA PAUL POGBA

KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba amekerwa na taarifa anazodai ni za upotoshaji zinazoelezea kuhusu tabia yake wakati akiichezea timu ya Juventus.

Pogba alitumia muda wa miaka minne akiitumikia klabu hiyo ya Turin na kuiwezesha kutwaa mataji ya Ligi ya serie A kila msimu kabla ya Agosti mwaka huu kuhamia Old Trafford kwa ada iliyovunja rekodi.

Hata hivyo, inasemekana kuwa wakati akiondoka alidai kuwa ni kama anakwenda mapumziko baadae atarejea, lakini kwa upande wake anadai kuwa hajawahi kuzungumza kitu kama hicho.

“Siku chache zilizopita niliulizwa kuhusu ninavyojisikia katika jiji la Manchester na wala sio kuhusu klabu,” alisema kiungo huyo mshambuliaji.


“Nimekuja Manchester United kwa sababu ni klabu ambayo nimekulia na nilikuwa najisikia narudi nyumbani,” aliongeza staa huyo.

No comments