TAMASHA LA X-MAS MORO LAINGIA DOA …FM, JAHAZI, MELODY WAJITOA, SIKINDE NAO MASHAKANI


TAMASHA kubwa la muziki wa taarab na muziki wa dansi litakalofanyika siku ya X-Mas mjini Morogoro limeingia doa baada ya bendi kadhaa kutangaza kujitoa.

Tamasha hilo ambalo limepangwa kufanyika katika Uwanja wa Jamhuri, lilitarajiwa kupambwa na Jahazi Modern Taarab, East African Melody, Ogopa Kopa, Wakali Wao, FM Academia, Sikinde na Msondo Ngoma. 

Jahazi Modern Taarab wametangaza kujitoa na badala yake watafanya onyesho lao jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Equator Grill huku FM Academia nao wakiiambia Saluti5 kuwa watakuwa Meeda Club, Sinza.

Kundi la Esat African Melody nalo limesema halitakwenda Morogogo kushiriki onyesho hilo na badala yake litatumbuiza Dar es Salaam.

Viongozi wa bendi hizo tatu wameiambia Saluti5 kuwa wamevunja safari ya Morogoro baada ya mwaandaaji kushindwa kumalizia malipo kinyume na mkataba wao.

Viongozi wa Sikinde nao wamesema hawana uhakika wa kwenda Morogoro labda tu mwaandaaji awakamilishie malipo yao kabla hapajapambazuka kuamkia siku ya onyesho.

No comments