TANGA KUIFANYIA ‘LISTENING PARTY’ MASHUJAA BAND SIKU YA X-MAS


WAKAZI wa mji wa Tanga watakuwa watu wa kwanza kusikiliza nyimbo mpya nane za Mashujaa Band ambayo ilikuwa kambini kwa muda mrefu.

Hatua hiyo itakuja kupitia onyesho maalum la bendi hiyo litakalofanyika mjini humu siku ya X-Mas Jumapili ijayo ndani ya ukumbi wa Nyumbani Hotel.

Kwasasa Mashujaa wameshaachia kete yao ya kwanza “Thamani ya Mapenzi” ambayo inatesa kwenye vituo vya radio, lakini ni wakazi wa Tanga ndiyo watakao kuwa wa kwanza kufaidi ‘live’ wimbo huo pamoja na zingine saba ambazo hazijasikika popote pale.

Mkurugenzi wa Mashujaa Band Maxi Luhanga ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo pia litamtambulisha rasmi mwimbaji Patient (Pasia) Budas kama rais mpya wa Mashujaa Band.

Aidha, Mashujaa pia itatambulisha wasanii wake wapya wakiwemo Facebook, Kandolo, John na James.
Patient Budas mwimbaji na rais mpya wa Mashujaa Band

No comments