THEO WALCOTT AIPA UBINGWA ARSENAL MSIMU HUU

WINGA wa Arsenal, Theo Walcott amekiangalia kikosi cha msimu huu na namna kinavyoendelea kufanya vyema na sasa anasema ana asilimia kubwa kwa timu yake hiyo kutwaa uchampioni wa msimu huu.

Kauli ya Walcott inakuja katika mazingira y Ligi ya Primier ya sasa ambapo “The Gunners” wamekuwa wakipotezana usukani wa kukaa kileleni na Chelsea.

Lakini straika huyo ameweka bayana kuwa kadri Ligi inavyoendelea anaamini Arsenal watatwaa ‘ndoo’ ya ubingwa.

“Sababu ya kutwaa ubingwa msimu huu tunazo tunapambana kwa ajili ya kujipanga kuhakikisha tunafanya vizuri katika kila mchezo na dhamira yetu ya sasa inabakia kuwa hivyo.”

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Southampon mwenye umri wa miaka 25 amesema kuanza kwa kipigo ni changamoto ya timu hiyo na kwamba anaamini kila jambo litakwenda sawa kwa Arenal ifikapo mwisho wa msimu ujao.

“Naamini kwamba kikosi hiki kinaweza kufanya makubwa zaidi ya yale ambayo yamewahi kufanyika huko nyuma ni kikosi imara sana,” amesema.


“Lakini unaona kwamba kila wakati tumekuwa tukiporomoka na kuyumba mimi nadhani sasa tuko vizuri zaidi ya huko nyuma yatupasa tuwe na imani hiyo,” amesema.

No comments