TIMU VIGOGO ENGLAND NI SHEEDAH KWA “SPECIAL ONE” MOURINHO

WAKATI Chelsea imeendelea kuvisambaratisha vigogo vya Ligi Kuu England, bado mambo ni magumu kwa kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ambaye amekwama kuvifunga vigogo msimu huu.

Mourinho amesimamia mechi 2 za Manchester United msimu huu nab ado timu yake imekuwa ikitamba dhidi ya zile za kawaida maarufu kwa jina la “mchekea.”

Pamoja na Manchester United kushika nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu, haijashinda kigogo chochote msimu huu.

Manchester United ilifungana bao 1-1 na Everton ambayo ni miongoni mwa timu ngumu kwenye Ligi Kuu England.


Timu hiyo imefungwa na Manchester City na Chelsea wakati ikiambulia sare ya vigogo vingine vya Arsenal na Liverpool.

No comments