TUNDAMAN ASEMA "KIKI"KWAKE SIO ISHU KABISA

TUNDAMAN amesema kuwa hana mpango na “kiki” kama afanyavyo baadhi ya wasanii kwa vile anaamini kuwa haziwezi kumsaidia kupiga hatua moja kwenda mbele.

Msanii huyo alisema kuwa ameamua kuweka azi msimamo wake huo baada ya kuwepo kwa maneno kwamba picha aliyoweka kwenye wimbo wake wa “Debe Tupu” ni kama anafanya uchokozi ili ajiongezee umaarufu.

“Nimesema tu kwa kifupi kuwa mimi sio mtu wa “kiki”, hata hilo kava la wimbio wangu wa “Debe Tupu” halijamlenga msanii yeyote maarufu kama ambavyo imekuwa ikidaia,” amesema.

Kwenye kava hilo kuna picha ya paka ambaye anajiangalia kwenye kioo lakini anajiona ni simba.

No comments