TWANGA PEPETA SASA KUFUNGA MWAKA MANGO GARDEN IJUMAA YA DISEMBA 30


HATIMAYE Twanga Pepeta imeamua kuaga mwaka na wapenzi wao wa Mango Garden, Kinondoni Ijumaa, Disemba 30.

Hapo awali Twanga Pepeta ilikuwa isionekane tena Mango Garden kwa mwaka huu baada ya kuwa ‘booked’ kwa Jumamosi zote zilizosalia mwaka huu.

Hata hivyo meneja wa Twanga Pepeta, Hassan Rehani, ameiambia Saluti5 kuwa kufuatia maombi ya mashabiki wao wengi, wameamua kufanya onyesho maalum Ijumaa ya wiki ijayo ndani ya Mango Garden.

Jumamosi hii Twanga watakuwa Songea na Jumamosi ya wiki ijayo - mkesha wa mwaka mpya, bendi hiyo itakuwa Dodoma.

No comments