TWANGA PEPETA YAKUMBWA NA HOMA YA EXTRA BONGO


MASHABIKI wa Twanga Pepeta wamekumbwa na homa kuzaliwa tena kwa bendi Extra Bongo.

Tetesi zimezagaa kuwa huenda Ally Chocky akaifufua tena Extra Bongo na kuachana na Twanga Pepeta, hii ni baada ya msanii huyo kufanya vizuri kwenye onyesho lake la kutimiza miaka 30 ndani ya muziki wa dansi.

Katika onyesho hilo lililofanyika Mango Garden Kinondoni Jumamosi ya Novemba 27, moja ya vitu vilivyokuwa kivutio ni ule wasaa wa Chocky kupiga nyimbo za Extra Bongo.

Tayari Chocky amepata show kadhaa mikoani katika mwendelezo wa shangwe za kutimiza miaka 30 kwenye ‘game’.

Hatua hiyo imezua mashaka makubwa kwa mashabiki wa Twanga na hata kwa baadhi ya viongozi wa bendi hiyo ambayo ina wasanii wengi waliowahi kuitumikia Extra Bongo.

Hata hivyo siku chache zilizopita Chocky aliiambia Saluti5 kuwa ana mkataba na Twanga Pepeta hadi mwaka 2018 na hana fikra za kuukatisha mkataba huo.

No comments