UMEMSIKIA JOSE MOURINHO?... asema eti Chelsea inabebwa ili kuziumiza timu nyingine kama man United

CHELSEA wanaitafuna Sikukuu ya Krismasi wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi Kuu ya England kwa tofauti ya pointi sita dhidi ya wanaoshika nafasi ya pili na pointi 13 dhidi ya Manchester United – timu inayofundishwa na kocha wa zamani wa Blues, Jose Mourinho.

Lakini Mourinho, kocha aliyejipachika jina la utani “Special One” anakosoa uwezo wa timu yake ya zamani, Chelsea akidai inabebwa.

Kocha huyo Mreno amesema: “Blues wamebebwa baada ya kupewa muda mwingi wa kupumzika kwenye ratiba ya Ligi Kuu England katika kipindi cha Sikukuu za mwisho wa mwaka.”

Mourinho amehoji kitendo cha Manchester United kupangiwa mechi nyingi kuliko timu yake ya zamani ya Chelsea kwenye ratiba ya mechi za Sikukuu.

Manchester United inatakiwa kucheza mechi tatu katika kipindi hiki tofauti na Chelsea ambayo imepangiwa kucheza mechi mbili tu.

Mourinho alisema timu yake itacheza kesho na Sunderland, mkesha wa mwaka wa mwaka mpya itakabiliana na Middlesborough wakati januari 2, imepangwa kuvaana na Westham.

Chelsea inakabiliana kesho na Bournemouth kisha mkesha wa mwaka mpya itapambana na Stoke City.

Hata hivyo itapumzika hadi Januari 4 mwakani ambapo Tottenham Hotspur.

“Ratiba hii ngumu ya Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya ni kwa ajili ya kuumiza baadhi ya timu kama zetu, kwa jinsi ratiba ilivyopangwa ni wazi ni kwa ajili ya kuadhibu baadhi ya timu wakati mwingine zinabebwa kwa kupewa mapumziko ya kutosha,” alisema Mourinho.


Mourinho alisema kuwa hata hiyo wameshazoea hali hiyo kwani pamoja na timu yake kucheza mechi za Kombe la Europa siku za Alhamisi, bado imekuwa ikipangiwa mechi za karibu karibu bila ya kupata muda wa mapumziko.

No comments