VILLAREAL YAWEKA PAUNI MIL 18 MEZANI KUMKAMATA BAFETIMBI GOMIS WA SWANSEA

VILLAREAL sasa iko tayari kuweka mezani kitita cha pauni mil 18 kwa ajili ya kumnasa straika wa Swansea, Bafetimbi Gomis.

Straika huyo raia wa Ufaransa ameingia katika rada za PSG inayotaka kuendeleza ubabe katika ligi ya Italia.

Dalili za Bafetimbi kutua katika kikosi cha Villareal zinatokana na kiwango chake kwa sasa kuwavutia baadhi ya wakala wa klabu mbalimbali.

Tayari Vallereal wamekutana na wakala wa nyota huyo na kwamba hata Swansea wenyewe wamwetibitisha taarifa za kuweko kwa pirika kuhusiana na straika huyo.


Timu hiyo ya La Liga imemthaminisha Mfaransa huyo kuwa ni wa dau la mil 18, ingawa wameonyesha dalili za kukubali kushusha kiwango.

No comments