WAZIRI WA FEDHA HISPANIA AMKOMALIA RONALDO TUHUMA YA KUKWEPA KODI


WAZIRI wa fedha wa Hispania, Jose Enrique Fernadez de Moya ametaka serikali ya nchi hiyo iachiwe kuchunguza tuhuma dhidi ya Cristiano Ronaldo za kukwepa kodi.

Moya alisema wamelipa uzito suala hilo baada ya kuibuliwa kwa tuhuma hizo dhidi ya staa huyo wa Real Madrid.

Alishauri wizara yake iachiwe kuchunguza tuhuma hizo dhidi ya Ronaldo.

Ronaldo hivi karibuni alitajwa kuwa miongoni mwa mastaa waliofungua akaunti za siri katika visiwa vya Virgin nchini Uingerza kwa ajili ya kupitisha mapato yao ya siri kwa ajili ya kukwepa kodi.

No comments