WEMA SEPETU YU MBIONI KUIHAMA TANZANIA NA KWENDA KUISHI KENYA

KAMA ndivyo alivyodhamiria basi huenda nyota Wema Sepetu akahamia nchini Kenya kwavile anaamini kwamba huko kunaweza kumfaa.

Miss Tanzania huyo wa zamani na mwigizaji nyota wa Bongomuvi aliposti hayo kwenye instagramu na inaonekana kuwa Kenya inaweza kuwa sehemu nzuri kwake na kuendesha shughuli zake.

Inawezekana msanii huyo atakuwa amechoshwa na maisha ya skendo akiwa nchini Tanzania na sasa amenza kufikiria kuanzisha maisha katika nchi nyingine na hasa Kenya ambako pia anpendwa sana.


Kuna wakati aliweka posti kwenye mtandao akiaga mashabiki wake wa Dar es Salaam akisema kuwa anahamishia makazi yake jijini Arusha, hata hivyo hakuamia huko.

No comments