WENGER AKIRI ALIHOFIA MARA YA KWANZA KUMCHEZESHA ALEXIS SANCHEZ KAMA MSHAMBULIAJI WA KATI

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger alihofia mara ya kwanza kuwa alikuwa anakosea kumchezesha Alexis Sanchez kama mchambuliaji wa kati.

Wenger alimchezesha kwa mara ya kwanza kwenye nafasi hiyo mwaka 2014 kwenye mechi dhidi ya Everton, ingawa alimtoa wakati wa mapumziko baada ya kujiona alikuwa amekosea.

Hata hivyo, Wenger amevuna matunda ya uamuzi wake na anaamini kuwa Sanchez ndie mrithi wa nyota wa zamani wa timu hiyo, Thiery Henry.


Sanches ambaye katika siku za karibuni amekuwa mfungaji tegemeo wa Arsenal anafanana na Henry kwa uwezo wake wa kufunga, kutoa pasi, chenga na mbio.

No comments