WENGER: WEST HAM ITACHUKUA HADI MIAKA MIWILI KUKAA SAWA

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa itachukua miaka miwili kwa timu ya Westham kukaa sawa kutokana na hali mbaya inayoikabili klabu hiyo ya jijini London.

Baada ya kukaa kwa miaka 112 ikitumia uwanja wa Upton Park, Westham msimu huu imeamua kuhamia kwenye uwanja wenye uwezo wa kuchukua idadi kubwa uliopo jijini Londan lakini imejikuta ikishindwa kufanya vizuri katika michuano ya Ligi Kuu England.

Jumamosi Westham ilijikuta ikifungwa kwa mabao 5-1 na Arsenal na hivyo kuporomoka hadi nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Ligi Kuu huku ikiwa mbele kwa pointi moja kutoka kwenye mstari wa kushuka daraja.

Kutokana na hali hiyo, Wenger ambaye alihama na Arsenal na kwenda nayo Emirates mwaka 2006 wakitokea Highbury alisema kuwa Westham inahitaji muda ili kuuzoea uwanja huo mpya.

“Inaweza kuchukua mwaka mmoja,” alisema Wenger.
“Pia huenda ukatumia hata miaka miwili iliuweze kukaa sawa kwa sababu unakuwa unatengeneza historia,” aliongeza Mfaransa huyo.


Alisema kwamba, katika uwanja wa Upton Park mashabiki walikuwa wakikaa jirani na ikumbukwe miaka mitano iliyopita Man City na Arsenal zilikuwa zinakufa pindi zilipokuwa zikitia mguu kwenye dimba hilo.

No comments