WEZI WAVAMIA NYUMBA YA RAPHAEL VARANE NA KUHONDOMOLA MALI ZENYE THAMANI YA EURO 70,000

JUMATANO iliyopita wakati akichezea Real Madrid dhidi ya Borussia Dortmund katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, wezi walivamia nyumba ya Raphael Varane.

Mfaransa huyo atajutia kutoweka mfumo wa ulinzi wa kutumia king’ora, jambo ambalo alithibitisha mbele ya polisi wakati tukio hilo liliporipotiwa.

Kwa mujibu wa gazeti la El Mundo, vitu vyenye thamani ya euro 70,000 (sh. mil 164), pesa taslimu, nguo na thamani nyingine, viliibiwa kutoka katika nyumba hiyo iliyoko katika makazi ya kifahari jirani na La Moraleja.

Hasara kamili inaweza kubwa zaidi kwani mchezaji huyo amesema vitu vingi zaidi vinaweza kuwa vimepotea nab ado hajafanya ukaguzi zaidi kujua vyote vilivyoibiwa.


Katika mechi hiyo, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 na kuifanya Madrid imalize katika nafasi ya pili ya Kundi lao.

No comments