WILFRIED ZAHA AAMUA KUJITOSA TIMU YA TAIFA YA IVORY COAST

STAA Wilfried Zaha ameamua kujitosa kuichezea timu ya taifa ya Ivory Coast ikiwa ni baada ya kukiwakilisha kikosi cha timu ya taifa ya England.

Winga huyo wa timu ya Palace mara ya kwanza kuichezea timu ya taifa ilikuwa ni katika michezo miwili ya kirafiki ambayo England ilikutana na Sweden na Scotland mwezi Novemba 2012 na agosti 2013.

Hata hivyo nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye ni mzaliwa wa mji wa Abidjan amebaki akiwa huru kulichezea taifa lake kutokana na kuwa hajawahi kuichezea England katika mechi za mashindano.

Baada ya kuona hakuna uwezekano wa kuichezea tena England, Zaha Jumapili aliamua kucheza mechi za timu ya taifa akiwa na Ivory Coast na sasa amepania kucheza fainali za mataifa ya Afrika Januari mwakani.


“Mwingereza mwenye asili ya Ivory Cost Zaha kwa sasa ameamua kuichezea Elephants chini ya rangi ambako ndiko alikozaliwa,” alieleza taarifa.

No comments