WIMBO MPYA WA LUKAS PODOLSKI “HABARI YA MUJINI” UJERUMANI

LUKAS Podolski ameongeza chati wiki hii na si ile iliyotarajiwa na wengi.

Anafahamika kwa uwezo wake kwa kupitia magoli lakini si mabao yaliyomweka namba moja katika chati wiki hii straika huyo wa zamani wa Arsenal amefunga magoli matatu akiwa na Garatasay msimu huu hivyo kuna kazi kubwa inayohitajika kufanyika upande huo.

Lakini nyota huyo ametisha upande mwingine kabisa kwenye anga la muziki.

Akishirikiana na marapa Mo-Torres na bendi ya Cat Ballou, Podolski ameweka rekodi ya kutoa wimbo uliopakuliwa nchini Ujerumani ndani ya siku saba zilizopita.

Wimbo huo wa rapu uliowavutia wengi umebeba jina la “Liebe Deine Stadt” (Upende Mji Wako).

“Ni kama ndoto hiki kinachotokea sasa,” alisema Podolski ambaye alionekana akifanya vitu vyake katika mitaa ya mji wa Cologne katika video ya wimbo huo mpya.


“Napenda kuwashukuru nyote kwa sapoti yenu katika wimbo wa “Upende Mji Wako.” Sikutarajia mafanikio haya.”

No comments