Habari

YAH TMK MODERN TAARAB WAFANYA KWELI MPO AFRIKA… leo “kukichafua” Lekam Royal Hotel Buguruni

on

IKIWA
ni shoo yao ya pili tangu ilipoanzishwa, bendi ya mipasho ya Yah TMK usiku wa
jana kuamkia leo imeonekana kukonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliohudhuria
makamuzi yao ndani ya Mpo Afrika, Tandika Davis Corner jijini Dar es Salaam.
Salatu
5 iliyokuwepo eneo la shughuli ilishuhudia namna vijana wa kazi wakiongozwa na
Omary Teggo “Special One” walivyokuwa wakiwacharusha mashabiki kwa burudani
kali.
Vibao
kama vile; “Sina Pupa”, “Kibaya Kina Mwenyewe”, “Figisufigisu” na “Siwaguni
Wala Siwakohoi” vilionekana kuwakuna wengi zaidi katika shoo hiyo iliyopambwa
na Madada Sita, Dullah Yeyo na Duillah Makabila.
Katika
kusheherekea Sikukuu ya Krismasi, Yah TMK leo inatarajia kuunguruma ndani ya
kiwanja cha Lekam Royal Hotel, Buguruni Dar es Salaam kuanzia tatu unusu, kwa
mujibu wa Meneja wao, Muddy K.

Zifuatazo ni picha
tano za jukwaani uone jinsi vijana hao walivyokamua ndani ya Mpo Afrika hapo jana.

 Waimbaji wa Yah TMK wakiwajibika jukwaani kwa raha zao
 Mpapasa kinanda mahiri, babu ally akifanya yake
Mameneja wa Yah TMK, Muddy K (kushoto) na Said Kessy Mnayama wakifuatilia kazi ya vijana wao kwa umakini mkubwa  
Mwimbaji Omary Teggo akiwadatisha mashabiki kwa songi lake jipya liitwalo “Figisufigisu Zimekwisha”
Mtaalam wa kinanda Rashid Yusuph “Chiddy Boy” naye akionyesha umahiri wake

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *