YAH TMK MODERN TAARAB YAINGIA RASMI KAZINI …Ijumaa wapo Kigamboni, X-Mas ndani ya Lekam Buguruni


KUNDI jipya la miondoko ya taarab Yah TMK Modern Taarab limeweka wazi ratiba yake ya msimu wa sikukuu ya X-Mas.

Ijumaa hii kundi hilo ambalo lilizinduliwa rasmi Jumamosi iliyopita, litakuwa CCM Kigamboni wakati Jumamosi ya mkesha wa X-Mas itakuwa ni zamu ya wakazi wa Tandika ndani ya ukumbi wa Mpo Afrika.

Mmoja wa wakurugenzi wa kundi hilo, Omar Teggo ameiambia Saluti5 kuwa siku ya X-Mas Jumapili hii, Yah TMK itafanya vitu vyake Lekam Royal Hotel Buguruni huku Boxing Day (Jumatatu) watakuwa Lunch Time Hotel Manzese.


Tayari Yah TMK imeshaachia nyimbo nne hewani ambazo zimekuwa gumzo: “Sina Pupa” wa Bi Mwanahawa Ali, “Kibaya Kina Mwenyewe” wa Aisha Vuvuzela, “Figisu Zimekwisha” ulioimbwa na Omar Te ggo na“Siwaguni wala Siwakohoi” wa kwake bibie Fatma Mcharuko.

No comments