YAH TMK MODERN TARAB YAHESABU MASAA TU KUJIANIKA DARLIVE KESHO JUMAMOSI

USIKU wa kesho Jumamosi unaweza kuwa wa historia nyingine kwa mashbiki wa mipasho pale bendi mpya ya taarab ya Yah TMK Modern itakapojianika mbele ya mashabiki na wadau.

Tukio la uzinduzi wa Yah TMK limepangwa kurindima ndani ya Darlive, Mbagala Zakheem, jijini Dar es Salaam kuanzia mishale ya saa 2:30 na kuendelea hadi majogoo huku wasanii kibao wakipamba shughuli hiyo.

“Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta”, Madada Sita, Dullah Yeyo, Leyla Rashid, TMK Wanaume na Dullah Makabila, wanatarajiwa kupamba shoo yetu ya utambulisho,” anasema Said Fella, bosi wa Yah TMK na ambaye pia ni diwani wa Kilungule.

Fella anasema kuwa anaamini shoo hiyo itakuwa funika bovu kutokana na maandalizi makubwa waliyoyafanya na anawaomba mashabiki wahudhurie kwa wingi kwa kiingilio cha sh. 10,000 tu mlangoni.


Yah TMK inaundwa na wasanii wengi mahiri kama vile Mwanahawa Ali, Maua Teggo, Omary Teggo na Amina Mnyalu, bila kusahau wale wengine waliotokea Jahazi Modern Taarab ambao ni Fatma Mcharuko, Aisha Vuvuzela, Mohammed Mauji, Mussa Mipango, Rashid Yusuph na Babu Ally.

No comments