YAH TMK WAENDELEA KUPASUA ANGA… wamimina bonge la shoo kwa mashabiki wa Bugurudi

YAH TMK Modern Taarab wameendelea kudhihirisha kuwa wamekuja kikazi zaidi kwenye tasnia ya mipasho baada ya jana Jumapili kupiga shoo yao ya tatu iliyokuwa kali zaidi, ndani ya Lekam Royal Hotel, Buguruni, Dar es Salaam.

Shoo ya kwanza ya bendi hiyo ilikuwa ni ile ya utambulisho iliyopigwa hivi karibuni ndani ya Darlive, Mbagala Zakheem na ya pili ni ile ya mkesha wa Sikukuu ya Krismasi iliyodondoshwa usiku wa juzi kuamkia jana Mpo Afrika, Tandika Davis Corner, Dar es Salam.

Miongoni mwa mambo yaliyoonyesha kuwa bendi hiyo “haiko kimchezo mchezo” ni burudani kabambe lililoungurumishwa na kukosha nafsi za mashabiki wao waliokuwemo ukumbini.


PATA PICHA ZA TUKIO LILIVYOKUWA:
Mwimbaji Amina Mnyalu akitoa burudani kwa mashabiki
Aisha Vuvuzela akiwa kazini
 Mcharaza gitaa la solo, Father Mauji akiwajibika
Hapa Maua Teggo akiimba kwa hisia
Chipukizi Jezza Mipango nae akisababisha

No comments