Habari

YAYA TOURE ANOGEWA NA MANCHESTER CITY …ataka iwe klabu kubwa kuliko Manchester United

on

KIUNGO wa Manchester City Yaya Toure anaangalia uwezekano wa kurefusha mkataba wake wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo baada kuimarika kwa uhusiano kati yake na kocha Pep Guardiola.
City inaonekana kama vile haikuwa na mpango wa kuendelea kuwa na nyota huyo wa Ivory Coast baada ya mkataba wake wa sasa unamwingizia pauni 230,000 kwa wiki kufikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu huku kiungo huyo akifikisha umri wa miaka 34.
Hata hivyo, kiwango anachoendelea kukionyesha Toure tangu arejeshwe uwanjani na Guardiola baada ya kuomba radhi kwa kauli za wakala wake Dimitri Seluk, kinaweza kushawishi mazungumzo mapya.
City imeshinda mechi zote tano ambazo Toure ameanza na sasa anaonekana atakuwa na nafasi kubwa kucheza kikosi cha kwanza baada ya kuumia kwa Ilkay Gundogan ambaye atakosa sehemu ya msimu mzima iliyoobakia.
“Wakati nilipojiunga na City, nilikuja katika klabu hii kuandika historia mpya,”alisema Toure. “Nataka klabu hii iwe kubwa kuliko Manchester United. Najua ni kazi kubwa lakini hiyo ndiyo njozi yangu.
“Nataka kufanya kitu muhimu sana. Tayari nimeshinda mataji mawili ya Premier League na nataka zaidi ya hapo, nahitaji historia mpya.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *