YOUNG KILLER ASEMA WASANII WA HIPHOP HAWAWEZI KUWA NA BIFU KUTOKANA NA MAFANIKIO YAO KIDUCHU

RAPA Young Killer amefunguka na kusema kuwa wasanii wa HipHop hawawezi kuwa na bifu kwa sababu wana mafanikio madogo kwenye muziki tofauti na wenzao wanaoimba.

Young aliiambia eNew kuwa hakuna msanii wa HipHop mwenye mafanikio ya kupata shoo ya sh. mil 10 ndiyo maana wanakosa cha kujitambia kwa madai kwamba bifu ningi husababishwa na mafanikio makubwa japo bifu zao zipo moyoni.


“Muziki wa sasa unachangamoto na ili upate nafasi ni lazima uzungumziwe hivyo sioni tatizo kutupiwa dongo na Stamina kwa hata paka sasa wanarapu,” alisema.

Msanii huyo aliongeza kuwa kwa sasa anajipanga kurudi na kurekebisha kila kitu ambacho anadhani hakipo sawa ili kuhakikisha anasimama imara bila kuyumba.

No comments