AFANDE SELE ASEMA SIA AJABU KWAKE KURUDI KWENYE GEMU

RAPA mkongwe, Selemani Msindi “Afande Sele” amesema kuwa uamuzi wake wa kurudi rasmi kwenye muziki sio wa ajabu na kuwataka mashabiki waendelee kumuunga mkono ingawa awali alikuwa amepanga kujikita zaidi kwenye kilimo.

Amesema kuwa baada ya kukosa ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 alitangaza kuacha siasa na muziki na kupanga kujikita kwenye kilimo lakini ameona ni bora arudi kwenye muziki kufanya kile ambacho mashabiki wanakitaka.


Mkongwe huyo amesema kuwa ameshaandaa kazi mpya ambayo anajiandaa kuitoa ikiwa ni ya kwanza baada ya kimya cha muda mrefu tangu alipojiingiza kwenye siasa na kuwania ubunge wa jimbo la Morogoro Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo.

No comments