AISHA MTAMUKABISA WA WAKALI WAO AVAMIA JUKWAA LA JAHAZI NA KUIMBA HASIDI HANA SABABU

MWIMBAJI Aisha Mtamukabisa wa Wakali Wao Modern Taradance Jumapili alivamia jukwaa la Jahazi Modern Taarab na kuimba kibao “Hasidi Hana Sababu.”

Tukio hilo lililovuta hisia za wengi lilitokea ndani ya ukumbi wa Lekam Loyal ambako wana Jahazi hurindima kila wiki katika siku za Jumapili.

Kitendo cha Aisha kupanda jukwaa la Jahazi na kusalimia kisanii kwa kuimba kimekuja kuondoa dhana kwamba bendi hizo zipo katika mgogoro mkubwa, hasa baada ya baadhi ya wasanii kuchomoka Jahazi na kuhamia Wakali Wao.

No comments