ALEXIS SANCHEZ APATA MRITHI NDANI YA ARSENAL... ni kinda wa miaka 17 kutoka Chile

ARSENAL imempa nafasi ya kufanya majaribio yosso wa miaka 17 kutoka taifa la Chile, Marco Allende wakiamini kuwa ndie atakuwa mrithi wa nyota wa klabu hiyo, Alexis Sanchez.

Sanchez anatoka Chile kama Allende ambaye wiki ijayo anajiunga na kikosi cha yosso cha Arsenal.

Allende ni miongoni mwa wanasoka wanaochipukia katika bara la Amerika Kusini na alicheza Chile kwenye michuano ya dunia ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2015.


Yosso huyo alikuwa anatarajiwa kuwasili jijini London wiki ijayo tayari kwa kujiunga na timu ya yosso ya Arsenal.

No comments