ANCELOTTI APANIA KUMNG’OA RAHEEM STERLING MANCHESTER CITY

BOSI wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti ameonyesha nia ya kupiga hodi katika klabu ya Manchester City kwa ajili ya kumwania kinda Raheem Sterling.

Mabingwa hao watetezi wa Ujerumani wameweka nia hiyo baada ya kuona bado kuna nafasi ya kumnasa straika huyo wa matajiri wa jiji la Manchester licha ya mara kadhaa straika huyo kukataa katakata kucheza soka la nje ya England.

Lakini Carlo Ancelotti amenukuliwa akisema anamwania kinda huyo kwasababu anatambua mchango wa wachezaji wa premier.

“Nina uhakika na wachezaji wanaocheza Ligi ya premier kwasababu ni Ligi ya mchakamchaka inayofanana na Bundesliga.”


“Raheem Sterling ni aina ya wachezaji ambao wanaweza kucheza katika Ligi yoyote kutokana na umri wake na hata aina ya kiwango alichonacho,” alisema Ancelotti.

No comments