ARSENAL KUM-SURPRISE SANCHEZ KWA BANGO LA PICHA YAKE NA MBWA LEO UWANJANI EMIRATES

ALEXIS Sanchez atashangazwa atakaposhuka kuitumikia Arsenal dhidi ya Burnley kwenye uwanja wa Emirates leo.

Sanchez atakapoingia uwanjani leo atakutana na bango kubwa lenye picha yake akiwa na mbwa wake wawili; Atom na Humber.

Arsenal ilitumia ukurasa wake wa Instagram juzi jioni kuposti picha ya bango hilo jipya kwenye uwanja wa Emirates.

Kikundi cha mashabiki wa Arsenal kiitwacho “REDaction” ambacho huhusika na kuboresha hali ya uwanja, ndicho kilichotoa wazo la kuweka bango hilo.


Bango hilo linatarajiwa kuwekwa ili kumbembeleza Sanchez ambaye hajasaini mkataba mpya na anahusishwa na mipango ya kutimka klabuni hapo, amwage wino.

No comments