Habari

ARSENAL YAPONEA TUNDU LA SINDANO KWA BOURNEMOUTH …Sanchez, Lucas Perez na Giroud waokoa jahazi

on

ARSENAL imeponea tundu la sindano baada ya kutoka nyuma 3-0 kabla ya kusawazisha na kuambulia pointi moja dhidi ya Bournemouth katika mchezo mkali wa Ligi Kuu ya England.
Hadi dakika 20 kabla mpira haujaisha, Arsenal walikuwa wameshakandamiziwa bao 3-0 kupitia kwa Charlie Daniels aliyefungua kitabu cha magoli dakika ya 16, Callum Wilson aliyepigilia la pili dakika ya 20 na  Ryan Fraser aliyemtungua Petr Cech dakika ya 58.
Wakati wengi wakianza kuamini kuwa Arsenal itarejea London bila hata pointi moja, Alexis Sanchez akaifungia bao la kwanza dakika ya 70, kabla Lucas Perez  hajatupia la pili dakika tano baadae.
Olivier Giroud akiwezesha Arsenal kuambulia pointi moja kwa bao lake la kichwa la dakika za majeruhi.
Bournemouth: Boruc, Francis, Steve Cook, Ake, Daniels, Arter, Gosling, Stanislas, King (Surman 63), Fraser (Adam Smith 68), Callum Wilson (Brad Smith 90).
Arsenal: Cech, Bellerin, Mustafi, Koscielny (Gabriel 64), Monreal, Coquelin (Oxlade-Chamberlain 28), Xhaka, Ramsey, Sanchez, Iwobi (Lucas Perez 63), Giroud
Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *