ARSENE WENGER AMPASHA OZIL “UNATAKA DAU NONO, BASI KAZA DOGO!”

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amemtaka staa wake, Mesut Ozil kufunga mabao zaidi ili aongeze sifa miongoni mwa mastaa wa soka duniani.

“nimemwambia Ozil ajiongeze kwa kufanya vitu vikubwa ambavyo ana vipaji navyo. Nimemshauri afunge mabao zaidi,” alisema Wenger juzi kabla ya timu yake kuikabili Swansea City jana.

Ozil yuko katika miezi ya mwisho ya mkataba wake na mazungumzo ya kuongeza yanasuasua kutokana na kutaka mshahara mkubwa.


Wenger alisema kuwa Ozil anapaswa kuongeza mchango wake kwenye timu ili ahalalishe madai ya kutaka kulipwa dau kubwa.

No comments