ARSENE WENGER ATABIRI WAHINDI KUWA JUU KISOKA ZAIDI YA WACHINA

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa soka la India litakuwa juu kuliko ilivyo kwa China hivi sasa.

“Hawa India kwa maoni yangu ni vidume vilivyolala lakini katika siku za usoni watatisha na sio China,” alisema Wenger wakati akizungumzia suala la nyota wa Ligi Kuu England kukimbilia China kwa siku za karibuni.

Wenger alisema haoni Ligi Kuu China ikiwa tishio kwani ana uzoefu na soka la Japan.

“Japan nao walianza kwa mkwara Ligi yao na nilikuwa huko wakati nyota kama Gary Linekar walipokuja, lakini hakuna mtu mwenye muda nao siku hizi,” aliongeza Wenger.


Wenger anaona Wachina wamekurupuka kwani bado wana safari ndefu hadi kuanzisha Ligi yenye nguvu. 

No comments