BAADA YA KUICHAPA YANGA 4-0, SURE BOY ATAMBA SASA AZAM INAREJEA KWENYE MAKALI YAKE


KIUNGO Salum Abubakary “Sure Boy” (pichani juu) amesema sasa Azam FC inarejea kwenye makali yake, hiyo ikiwa ni baada ya kuichakaza Yanga 4-0 kwenye Kombe la Mapinduzi.

Jana usiku, Azam iliyokuwa ikionekana dhaifu kwenye michuano hiyo, iliifunika Yanga katika kila idara na kuiadhibu kirahisi 4-0 huku pia ikipoteza nafasi nyingi za wazi ambazo zingewawezesha kuvuna mabao mengi zaidi.

Baada ya mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Amani, Zanzibar, Sure Boy akatamba kuwa sasa wachezaji wa Azam (wengi wao wakiwa wapya) wameanza kushikana na hivyo mambo mazuri yanakuja.

“Wachezaji wengi ni wapya, wamesajiliwa katika nusu ya msimu huu, makocha nao ni wapya, kwahiyo timu ilikuwa haijashikana lakini sasa mambo yanaanza kuchanganya,” alisema Sure Boy, mtoto wa winga za zamani wa Yanga - Abubakary Salum "Sure Boy" Orijino.

No comments