BAADA YA "MARIO", BABY MADAHA SASA KUIBUKA NA KITU "KRAZON"

BAADA ya kuipua video ya wimbo “Mario” akiwa na kundi la Scorpion Girls, staa wa muziki wa Kizazi Kipya, Baby Madaha amesema kuwa anajiandaa kutoa mwingine binafsi uitwao “Korazon”.

“Huo utakuwa wimbo wangu wa kwanza kwa mwaka huu wa 2017 mimi kama Baby Madaha, hivyo mashabiki wangu wajiandae kupata kitu hicho wiki chache zijazo,” amesema.

Kuhusu video ya wimbo Mario, amesema kuwa ameimba na wasanii wenzake Isabella Mpanda na Jini Kabula ambaye sasa ameamua kuokoka na kuimba nyimbo za Injili.  


Amesema kuwa baada ya kumaliza video ya wimbo huo, Jini Kabula aliwaambia kwamba hataki tena kuimba muziki wa kidunia, hivyo amebaki yeye (Baby na Isabella) 

No comments