BABA RAHMAN AAGA RASMI MICHUANO YA AFCON... Waghana wasikitika kumpoteza

MLINZI wa Ghana, Black Stars “Baba Rahman” hatacheza tena michuano ya AFCON mwaka huu baada ya kuumia goti la kushoto katika mechi dhidi ya Uganda.

Mchezaji huyo mwenye miaka 22, anayeichezea Schalke 04 ya Bundesliga kwa mkopo akitokea Chelsea, amesafirishwa kwenda Ujerumani kwa ajili ya matibabu ya kina.


Uongozi wa Ghana ulisema unasikitika sana kumpoteza Rahman kwenye mechi zake zilizosalia za michuano hiyo ambayo wamepanga kutwaa ubingwa baada ya kuukosa mwaka 2015 walipotolewa na Ivory Coast kwa pointi.

No comments