BALE, BENZEMA NA RONALDO WASABABISHA "MAJANGA" REAL MADRID

KUTOCHEZA pamoja kwa nyota watatu wa Real Madrid kunaelezwa kuwa ndio chanzo cha kuboronga kwa vigogo hao katika siku za karibuni.

Kombinesheni ya mastraika hao watatu; Gareth Bale, Karim Benzema na Cristiano Ronaldo  imepachikwa kifupi cha “BBC” kutokana na majina ya washambuliaji hao.

Real Madrid juzi ilitolewa kwenye michuano ya Copa del Rey na Celta Vigo kiasi cha kuwapa wasiwasi mkubwa mashabiki wa timu hiyo.

Ronaldo inadaiwa amekuwa kama mpweke kwenye kikosi cha Real Madrid kutokana na nyota wenzake katika ufungaji Bale na Benzema kuwa majeruhi.


Wachambuzi wa masuala ya soka wanadai kuwa Real Madrid itakuwa na wakati mgumu ikiendelea kukosa kombinesheni ya “BBC”.

No comments