BAYERN MUNICH WAMPIGIA MAHESABU RAPHAEL VARANE

TAARIFA za tetesi za usajili mwishoni mwa juma lililopita zinamtaja nyota wa Real Madrid, Raphael Varane kuwa ana asilimia kubwa ya kuwindwa na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich.

Daily Star, imemwelezea Varane kama ni mchezaji wa awali aliye katika malengo ya Bayern Munich na tayari kuna hatua zinaendelea chini kwa chini. Kwamba wawili hao wameshaanza kuteta.

Verane amekuwa akikosa namba ya kudumu katika kikosi cha Los Brancos cha msimu huu baada ya kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane kuwapa nafasi kubwa walinzi Sergio Ramos na Pepe.

Varane mwenye umri wa miaka 23 ameelezwa kutoficha mapenzi aliyonayo kwa kutaka kukipiga katika Ligi ya nchini Ujerumani.

Hata hivyo, akinululiwa na Sky Sports kuhusiana na uvumi huu, kocha zidane amesema inawezekana kuna timu zinamwitaji Varane ikiwemo Bayern Munich, lakini taarifa za klabu yake hazina mpango wa kumruhusu aondoke.

“Varane ni kati ya wachezaji ambao ni hazina ya baadae kwa klabu yetu na sipo tayari kumuona akiondoka licha ya mazingira ya sasa ya kutopata nafasi ya kudumu katika kikosi,” alisema Zidane na kuongeza.


“Ninachofanya ni kumtaka Varane kujifunza kutoka kwa mabeki wazoefu kama Sergio Ramos na Pepe ili aje kuwa mzuri katika mechi kubwa kama za Ligi ya Mabingwa.”

No comments