BEKI BABA RAHMAN WA GHANA ARUDI UJERUMANI KUFANYIWA OPERESHENI YA GOTI

BEKI wa Ghana, Baba Rahman amerudi Ujerumani kwa ajili ya kufanyiwa operesheni ya goti baada ya kuumia kwenye fainali za Kombe la Mataifa Afrika.

Rahman mwenye umri wa miaka 22, amerudishwa kwenye klabu yake ya Schalke ambako anacheza kwa mkopo.

Beki huyo aliumia kwenye mechi ya fainali hizo dhidi ya Uganda.


Rahman amesajiliwa na Chelsea lakini msimu huu alipelekwa kwenda kucheza kwa mkopo Schalke.

No comments