Habari

BEKI VICTOR LINDELOF ANUKIA MANCHESTER UNITED KWA PAUNI MIL 38 …aandaliwa jezi No. 2, Bailly amsubiri kwa hamu

on


VICTOR LINDELOF amefanya makubaliano ya awali ya kujiunga  Manchester United kwa puani milioni 38, hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Express wa Uingereza.

Sentahafu huyo wa Benfica amekuwa akihusishwa na usajili wa kwenda United kwa muda mrefu na ingawa Mourinho amekanusha kuwa na mipango ya kufanya usajili katika dirisha dogo la Januari, lakini Sky Sports ya Uingereza nayo pia imeeleza kuwa makubaliano ya awali yamefanyika kwaajili ya nyota huyo wa Sweden kutua Old Trafford mwezi huu.
Lindelof atasaini mkataba utakaomwingizia mshahara wa pauni  115,000 kwa wiki na ameandaliwa jezi namba 2.
Beki wa kati wa United  Eric Bailly amesema anasubiri kwa hamu ujio wa  Lindelof  Old Trafford.
Akizungumza kwenye kambi ya African Nations Cup akiwa na timu ya taifa ya Ivory Coast, Bailly alisema: “Natarajia kucheza sambamba na yeye. Natumai atakuwa msaada mkubwa kwetu”.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *