BEN BRANCO AIKUMBUKA AJALI YA "KRISMASI" NA KUSEMA ILIKUWA AFE

MKALI wa filamu za vichwekesho, Ben Branco ameikumbuka ajali aliyoitapa siku ya Krismasi na kusema kwamba hakuamini kama angetoka salama na kuendelea kuwa hai hadi leo.

Ajali hiyo iliyohusisha gari ndogo aina ya Mark II Grand waliyokuwemo yeye, rafikize wawili na watoto wadogo watatu na Range Lover, ambayo yaligongana uso kwa uso, ilitokea majira ya saa 7:00 mchana wakiwa wanaenda kujirusha Beach.

“Ajali ile ilinifanya nipoteze fahamu na kurejewa na kumbukumbu nikiwa nimelazwa wadi namba 13, Kibasila, Muhimbili, huku nikiwa nimechanwa ubavu wa kulia na madaktari ili kutoa upepo uliokuwa umenijaa mapafuni na kunifanya nishindwe kupumua,” amesema.


Ben amesema kuwa hivi sasa anaendelea vizuri baada ya kulazwa hospitalini hapo kwa siku tano na kuruhusiwa, ambapo amewashukuru baadhi ya viongozi wa serikali, wasanii wenzake pamoja na mashabiki waliofika kumjulia hali na kumpa ushirikiano.

No comments