BEN SERENGO AIPA “SHIKAMOO” KOMEDI YAKE YA “LANGO LA JIJI”

MKALI wa Komedi za Kibongo, Ben Serengo amesema filamu ya “Lango la Jiji” ni kati ya kazi ambazo hatakaa azisahau kutokana na kwamba imempa heshima kubwa, licha ya kuwa ilikuwa ndio ya kwanza kwake.

Filamu hiyo ya vichekesho iliyoshirikisha nyota wengi wakiwemo yeye mwenyewe (Ben Serengo), Mtanga, Samofi, Mboto, Senga, Masanja Mkandamizaji na wengineo wengi, ilitoka mwaka 2008.


“Nitatengeneza kazi nyingi sana lakini sitaisahau ile ya “Lango la Jiji” kwasababu uwezo wangu ulianza kujianika pale na watu wakawa wanajua mimi ni nani katika sanaa,” amesema Serengo.

No comments