BORUSSIA DORTMUND WAMSARANDIA RAHEEM STERLING WA MANCHESTER CITY

MOJA ya vigogo vya Bundesliga, Borussia Dortmund wameonesha nia ya kupiga hodi katika klabu ya Manchester City kwa ajili ya kumwania Reheem Sterling bila kujali kama ameongeza mkataba mpya ama la!

Sterling aliingia katika mpango wa kutua Bayern katika usajili wa dirisha dogo la mwezi Januari mwaka huu na mkataba huo bado unawekwa mezani kwa ajili ya usajili wa majira ya kiangazi. 

“Nina uhakika wa wachezaji wanaocheza Ligi ya Premier kwasababu ni Ligi ya mchakamchaka inayofanana na Bundesliga.”

“Ninatambua pia ugumu uliopo wa kumnasa kinda huyo kutokana kuwa tegemeo kikosini mwake lakini naamini tutaketi mezani na kukubaliana na wenzetu wa Man City," kilieleza chanzo cha ndaniya Dortmund.


“Raheem ni aina ya wachezaji ambao wanaweza kucheza katika Ligi yoyote kutokana na umri wake na hata aina ya kiwango alichonacho."

No comments