CAF YAPEWA ONYO KUPELEKA MICHUANO YA MATAIFA AFRIKA GABON

SHIRIKISHO la soka barani Afrika CAF limelazimika kuomba msaada kutoka kwenye taasisi kubwa na za kimataifa za kupambana na uharifu wa mtandaoni.

Hiyo ni baada ya wahuni kuuteka mtandao wa Website wa CAF na kuutumia kuweka matangazo yao wakidai kuwa ni onyo kwa uamuzi wa Shirikisho hilo kuyapelea mashindano makubwa mjini Gabon huku wakijua kwamba nchi hiyo inatawaliwa kiimla.

Viongozi wa CAF kwa kushirikiana na maafisa usalama wa Gabon walifanya kila njia kuhakikisha wahuni hao hawaleti mahara kwenye mtandao huo.


“Gabon ni nchi inayotawaliwa kidikteta kwa hiyo hatuwezi kukubali kuona nchi kama hii ikipewa heshima kama hii na Afrika au na dunia,” ilisema taarifa ya kundi hilo.

No comments