CAMEROON YATOKOTA KESI YA KUMCHOMEA UTAMBI JOEL MATIP FIFA

SHIRIKISHO la Soka la Cameroon limeshindwa katika maombi yake ya kutaka Joel Matip azuiwe kuchezea Liverpool katika kipindi hiki cha fainali za Kombe la Mataifa Afrika.

Cameroon iliwasilisha malalamiko kwenye shirikisho la soka la kimataifa (FIFA), kulalamikia kitendo cha beki huyo kugoma kujiunga na timu yake ya taifa ya nchi hiyo kwenye fainali za Kombe la Mataifa Afrika.

FIFA ambayo ilitaka mara ya kwanza suala hilo limalizwe na pande hizo mbili, baada ya kuona hakuna mwafaka iliamua kuanza kulichunguza.

Baada ya uchunguzi wake, iliridhika kuwa Matip hakuwa na makosa na ameruhusiwa kuchezea Liverpool.


Matip alitangaza kutochezea timu hiyo kabla ya fainali hizo kuanza, kitendo ambacho kiliikasirisha Cameroon iliyopeleka malalamiko FIFA na kutaka beki huyo asicheze hadi fainali za Afrika zitakapomalizika.

No comments