CHILLAH KUPA AFRIKA KUSINI KUANDAA KICHUPA CHA “KOKU”

MSANII wa muziki wa Kizazi Kipya Q Chillah anatarajia kusafiri kwenda Afrika Kusini leo kwa lengo la kushuti video ya wimbo wake alioupa jina la “Koku” ili kukata kiu ya mashabiki wake.

Alisema kuwa video hiyo inafuata baada ile ya “Sungura” aliyoitoa Desemba mwaka jana ambayo bado inaendelea kutamba.

“Kama Mungu akinijalia ninatarajia kusafiri kwenda Afrika Kusini Januari 17 (leo), nikiwa na uongozi wangu nikafanye kazi moja tu ya kushuti video ya wimbo wangu ambao nimemshirikisha msanii Patoranking kutoka Nigeria,” alisema Chillah.


Msanii huyo alisema kuwa hakuwa na haraka ya kutoa video hiyo lakini amelazimika kufanya hivyo kwa vile mashabiki wake wanatamani kumshuhudia jinsi anavyofanya vitu vyake akiwa na Patoranking.

No comments